June 27, 2016


Kikosi cha TP Mazembe wamejifua kwa nusu saa tu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

TP Mazembe kutoka DR Congo wako nchini kuwavaa Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho, mechi itakayipigwa kesho kwenye uwanja huo.

Wachezaji wao walipoingia uwanjani hapo, walinzi walioongozana na kikosi hicho walianza kuzuia watu kuingia uwanjani hapo.

Walizuiwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi na inaonekana Mazembe walijifua haraka na kwa muda mfupi na baada ya hapo walipanda basi na kurejea hotelini.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV