June 27, 2016Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua hatacheza katika mechi ya Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikiivaa TP Mazembe.

Joshua ni majeruhi baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Mo Bejaia nchini Algeria. Nafasi yake ilichukuliwa na Haji Mwinyi ambaye naye alilambwa kadi nyekundu.

Kutokana na hali hiyo, Kocha Hans van der Pluijm atalazimika kumtumia Mbuyu Twite upande wa kushoto.


Tayari Yanga ina pengo la kiungo wake mwenye kasi, Simon Msuva ambaye ataikosa mechi hiyo kutokaba na kuwa na malaria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV