June 27, 2016


Wakati malumbano ya nani ataonyesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, sasa taarifa rasmi zimetolewa kuwa DStv wataurusha mchezo huo.

DStv kupitia Super Sport 9 East wataurusha mchezo huo moja kwa moja.

Meneja Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu amethibitisha kuhusiana na hilo, leo.

"Kweli Super Sport 9 East wataurusha mchezo huo moja kwa moja. Hivyo itakuwa nafasi nzuri kwa mashabiki nchini kufaidika.

"Ni mechi kubwa kwa Tanzania na Afrika kote, hivyo mashabiki waitumie nafasi hiyo kwa kuhakikisha wanalipia ving'amuzi vyao ili wasipitwe," alisema.

Yanga inaivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho ambayo mashabiki wataingia bila kulipa kiingilio.


Tayari mechi hiyo ni gumzo kwa kuwa mashabiki wa Yanga wataingia bila kiingilio na wametakiwa na uongozi wa Yanga kujitokeza kwa wingi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV