June 27, 2016

Uamuzi wa Lionel Messi kustaafu timu ya taifa ya Argentina ndiyo gumzo kubwa mitandaoni.


Wengi wanazungumzia uamuzi huo kuwa ni wa haraka au jazba baada ya Argentina kukosa ubingwa wa Copa Amerika baada ya kuchapwa kwa penalti 4-2 na Chile.

TAKWIMU:
113 - MECHI ALIZOICHEZEA Argentina.
MECHI YA KWANZA: vs Hungary 2005. 
MABAO: Ni 55, kati ya hayo matano alifunga kwenye Copa America 2016.

MICHUANO AKIWA NA ARGENTINA: Copa America 2007, 2015, 2016; World Cup 2014. 

MABAO AKIWA NA BARCELONA: Ni 453, anashikilia rekodi ya kufunga mabao 312 la Liga.
MAKOMBE LA LIGA: Amechukua ubingwa mara 8
UBINGWA CHAMPIONS LEAGUE: Amebeba makombe 4 

MCHEZAJI BORA WA DUNIA: Ameichukua mara tano, ndiyo mara nyingi zaidi kuwa FIFA Ballon d'Or player of the year. Miaka aliyochukua ni 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV