June 27, 2016


Mashabiki wa soka wametoa pongezi nyingi kwa StarTimes kutokana na kuonyesha mwanzo mwisho michuano ya Copa America.

Michuano hiyo iliyofanyika nchini Marekani, Chile ndiyo wameibuka mabingwa kwa kuwafunga Argentina kwa mabao 4-2 ya mikwaju ya penalti.

Mashabiki wengi wa soka waliotuma maoni yao kwenye salehjembe@gmail.com wamesema, pamoja na muda ‘mbaya’ wakati zikichezwa mechi hizo, StarTimes waliendelea kuwa na wanamichezo wa Tanzania.

Wengi wamesema bila ya StarTimes wangekosa mambo mengi sana ya msingi na faida kubwa ya namna soka katika ukanda wa Amerika lilivyo na ushindani wa juu.


Wengi wanaamini wamepata faida kubwa kutokana na michuano hiyo kuwa ya ushindani wa juu sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV