June 8, 2016


Nyota wa zamani wa Nigeria akiwa mchezaji na baadaye kocha,  Stephen Keshi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54.

Keshi aria wa Nigeria amefariki katokana na shambulizi la ugonjwa wa moyo na inaelezwa alianza kuumwa mguu.


Keshi, nahodha wa zamani wa Nigeria ni kati ya Waafrika wawili waliofanikiwa kubeba Kombe la Mataifa Afrika wakiwa wachezaji na baadaye kocha.


Pia amewahi kuwa kocha wa timu za taifa za Togo na Mali kwa nyakati tofauti. Keshi, aliwahi kucheza Ulaya na kutamba akiwa na klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV