June 8, 2016Baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta 'Popa' kukosa penalti katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri, baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Mzee Ally Samatta, amefunguka kuwa  ilikuwa lazima akose penalti hiyo kutokaana na kukosea hesabu zake kabla ya kuamua kupiga.

 Stars imepoteza matumaini ya kuweza kufuzu katika fainali hizo kwa mara ya pili baada ya mwaka 1980, kufuatia kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo huo uliopigwa Wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 Mzee Samatta alisema ilikuwa lazima nahodha huyo kukosa penalti ile kutokana na kukubali kudanganywa kizembe na kipa wa Misri, Essam  El Hadary.

“Nimesikitika Mbwana kukosa ile penalti lakini kwa upande wangu nilijua mapema lazima atakosa kwa sababu alikubali mapema kuongopewa na yule kipa (El Hadary), kutokana na kugundua mapema sehemu alipokuwa nataka kuleta mpira na ndiyo matokeo yake aliupaisha.

“Unajua hata kule Msumbiji yeye ndiyo alisababisha tukashindwa kufuzu baada ya kukosa penalti ya mwisho kwa mtindo kama ule wa kubadilisha maamuzi haraka kitu ambacho kinampa urahisi wa kipa kudaka na wakati mwingine kupaisha.

 “Hata yeye mwenye amekiri kuwa yule kipa aligundua sehemu atakayopiga akazidi upande ule na matokeo yake kosa na tayari ameshanieleza kulipa faini yake ya  Sh5000 kwa kosa la kukosa penalti yake,” alisema Mzee Samatta.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV