June 27, 2016


Baadhi ya mashabiki waliosema ni wanachama wa klabu ya Simba, wamejitokeza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu ya Yanga na kuwataka Wanasimba kujitokeza kwa wingi na kuiunga mkono Yanga, kesho.

Yanga inashuka dimbani kuivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Amaniel Mngonja na Rifat Maulanga wamejitokeza kwenye mkutano huo ulioongozwa na Msemaji wa Yanga, Jerry Muro katika makao makuu ya Yanga, Kaunda na Twiga jijini Dar es Salaam.

“Sisi sote ni mashabiki na wanachama wa Simba, tunawaomba mashabiki na wanachama wenzetu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Yanga.

“Yanga ndiyo inayoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo, hivyo waje kwa wingi kuishangilia,” alisema Maulanga.

Kwa upande wake, Muro alisema kwa shabiki ambaye hataweza kuvaa jezi za Yanga, angalau avae jezi za Taifa Stars.


“Kama utashindwa basi vaa jezi ya Taifa Stars, lakini bado unaweza kuvaa jezi ya timu yako hata kama ni Simba lakini beba bendera ya taifa, tuishangilie Yanga ni kwa ajili ya Tanzania.”

Kuhusiana na uanachama wa Simba wa Maulanga na Mngonja, wote walikataa kutaja kadi zao za uanachama na kusisitiza hawakuwanazo hapo.

4 COMMENTS:

  1. Imezoeleka kwa timu za Tanzania kuwa tunashangilia wageni,ndio sifa tulio nayo na hasa simba,sio Azam wala timu nyingine,na TP.Mazembe wamekuja wakijua watashangiliwa na simba ndio maana wamekuja na jezi za kumwaga na wanauza sana tu,Ukweli ni kwamba simba watashangilia TP Mazembe kama walivyofanya kwa waarabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tatizo lenu mnasahau sana kama mnakumbuka nyie yanga ndyo mlianza kimbelembele cha kushangilia wageni, mechi ya stella abidjan mliimba uzalendo umewashinda,TP mazembe pia mliwashangilia, vipi kuhusu FC libolo ya angola pia mlishangilia so acha tuende sawa Yanga siyo timu ya Taifa so kila mtu ashabikie timu anayoipenda

      Delete
  2. Haitokuja kutokea simba wakawashangilia yanga kamwe. Wamekaa na kuwavalisha wanachama wao jezi za simba na kujifanya hao ni mashabiki wa simba. Walianza acha yaendelee tu hakuna namna kwenye hili. Unoko mwenzake unoko tu

    ReplyDelete
  3. Kwa Tanzania hii hilo halipo,kama watu wanagawanyika hadi kwenye timu ya Taifa badala ya kuishangilia timu wanashangilia wachezaji waliotoka timu yao leo wataanzaje kushangilia mahasimu wao?Kama hilo likiwezekana litakuwa moja ya faida za kuzima simu feki,yawezekana simu feki zilikuwa zinasababisha mawazo feki na hulka feki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic