June 2, 2016


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ametua katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani na kuchukua rasmi fomu za kuwania uongozi, uchaguzi utafanyika Juni 11 jijini Dar es Salaam.

Manji amechukua fomu za kuwania uongozi sambamba na makamu wake, Clement Sanga.

Manji amepokewa kwa sherehe kubwa na mashabiki na wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kumshuhudia akichukua fomu.

Kiongozi huyo aliyeipa Yanga mafanikio makubwa, alizungumza na wanachama hao baada ya kuchukua fomu na kueleza mambo kadhaa likiwemo lile la tuhuma za hujuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV