June 2, 2016


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameeleza namna alivyosimamisha uanachama wa baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwemo wachezaji wa zamani kama Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ na Aaron Nyanda.

Nyanda na Malima ni wachezaji wa zamani wa Yanga ambao walikuwa kati ya waliochukua fomu za kuwania uongozi kupitia uchaguzi wa Yanga ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopangwa Juni 25.

MALIMA
Mwingine aliyevuliwa uanachama ni anayejulikana kuwa ni Mwenyekiti wa Matawi wa Yanga, Mohammed Msumi, cheo ambacho uongozi chini ya Manji umekuwa ukisisitiza hakipo kikatiba.

Lakini Manji akaeleza kulikuwa na njama za kumng’oa na kumuondoa zilizokuwa zikifanywa na baadhi ya wanachama wakiwemo baadhi ya maofisa wa TFF.

“Kweli nimewavua uanachama baada ya kugundua njama hizo. Kamati husika ya Yanga ambayo ni ile ya nidhamu itakaa na kulifanyia kazi hili.

“Kama itaona kuna tatizo, itakazia nilichokitangaza. Kama hawana tatizo, basi itabadili, tuiachie kamati,” alisema Manji.

NYANDA
Manji pia aliungana na wanachama waliungana kuwasikiliza sauti za watu aliowatuhumu kuwa ni baadhi ya wanachama wa Yanga na maofisa wa TFF waliokuwa wakipanga njama za kumng’oa kwa makusudi.

2 COMMENTS:

  1. Mie nadhan hawa waitwe wajieleze na waruhusiwe kuchukua fom Yanga,sidhan km wanakosa kuchukua TFF

    ReplyDelete
  2. Mie nadhan hawa waitwe wajieleze na waruhusiwe kuchukua fom Yanga,sidhan km wanakosa kuchukua TFF

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic