June 21, 2016Awali ilielezwa kwamba Yanga itarejea nchini mapema na kuachana na kambi ya Uturuki.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro akalitbithisha hilo! Lakini taarifa nyingine za uhakika zimesema Yanga itaendelea na kambi yake ya Uturuki.

“Kweli kambi ya Uturuki itaendelea kama kawaida,” kilieleza chanzo.

“Tayari timu ipo Uturuki na leo itafanya mazoezi jioni kuanza rasmi maandalizi ya TP Mazembe.”

Yanga ilianzia Uturuki katika mji wa Antalya, baada ya hapo ikasafiri kwenda kucheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho ambayo ilipoteza kwa bao 1-0.


Sasa imeanza maandalizi kwa ajili ya mechi yake ya pili ambayo itakuwa ni dhidi ya TP Mazembe pia ikiwa ni ya kwanza nyumbani na itapigwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV