June 21, 2016


Na Saleh Ally
Picha hii inaweza ikakupa sura ya maisha yanavyoweza kuwa magumu au baadaye kubadilika na kuwa bomba kabisa lakini lazima upambane.

Watanzania wengi wakiwemo wanamichezo, wanapenda sana mafanikio ya maisha bila ya kupambana hata kidogo. Watanzania wengi tunapenda sana kusukuma lawama kwa kila kitu.

Wengi wamekuwa wakifeli lakini angalia mfano huu, ndani ya miaka 10, Dimitr Payet ni mtu mwingine kabisa. Hii inaonyesha alikuwa akipambana muda mwingi wa maisha yake na kutaka kuhakikisha anashinda.

Payet sasa ni mmoja wa wachezaji nyota wanaoitumikia West Ham United, ni nyota wa Ligi Kuu England, nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa na gumzo kati ya wanaoshiriki michuano ya Euro 2016.

Mwaka 2006 alikuwa mfanyakazi wa dukani ambaye mshahara wake kwa mwezi usikufikia hata Sh milioni 1 na nusu. 

Mwaka 2016, Payet ni staa na analipwa mamilioni ya fedha na Sh milioni 1 na nusu si kitu kwake tena.

Hauwezi ukaniambia nikakubali kwamba mafanikio yake yametokana na kuomba dunia tu. Haiwezi kuwa rahisi hata kidogo kwake alitumia muda mwingi kulalamika halafu akafanikiwa.

Lazima tukubali kwamba maisha ni mapambano, juhudi na maarifa ni msingi na lazima kila mmoja ajipiganie kwanza na mengine yafuatie.


Payet anaweza kuwa sehemu ya mfano, kwani ndani ya miaka 10, maisha yake yamebadilika kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic