July 23, 2016


ZEBEN AKIWA MAZOEZINI NA AZAM FC

Kikosi cha Azam FC keshokutwa Jumatatu inakwenda Zanzibar kuweka kambi ya siku saba kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii na Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

Azam itaondoka na wachezaji wake wote wakiwemo watano wa kigeni wanaofanya majaribio na kikosi hicho kinachonolewa na Mhispania, Zeben Hernandez.

Zeben alisema kambi hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya kukipa makali kikosi chake ikiwemo kucheza michezo miwili ya kirafiki.

“Tunakwenda Zanzibar, Jumatatu ijayo na nitaendelea kuwachuja wachezaji wangu kwani nataka kubaki na kati ya wachezaji 20 mpaka 22 katika msimu ujao wa ligi,” alisema Zeben.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic