Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amezindua rasmi kikosi cha kuipandisha KMC FC katika Ligi Kuu Bara na moja ya mambo aliyofanya ni kumkabidhi jezi yake kiungo mpya wa timu hiyo, Athumani Iddi ‘Chuji’.
Chuji ambaye ni nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Mwadui FC amejiunga na timu hiyo tayari kabisa kuhakikisha msimu uhao inapanda daraja.
Pamoja na Chuji wengine ambao wamesajiliwa na KMC FC ni Eric Mawala (kutoka Mbeya city), Issa Ngoah (Simba), Rashid Roshwa (Kagera Sugar), Lembele Jerome (Kagera Sugar) na Mussa Kidu (JKT Ruvu).
0 COMMENTS:
Post a Comment