July 28, 2016


Kikosi cha Yanga kimerejea nchini baada ya kupoteza mechi yake ya tatu ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama nchini Ghana.

Yanga wametua nchini kwa mafungu, wakianza na kundi la kwanza lililotua jijini Dar es Salaam saa 8 usiku.

Baadaye saa 2 asubuhi, kundi la pili likiongozwa na kocha Hans van der Pluijm nalo likawasili.

Ingawa mashabiki wamekuwa wakijaribu kujipa moyo, lakini hali halisi hasa ni kwamba Yanga haina nafasi tena ya kufuzu hatua ya nusu fainali.

Kocha Pluijm, amesisitiza makosa ambayo waliyazungumza, yamefanyika na kuwafanya wapoteze mchezo.

Ingawa alilalamika suala la safari ndefu hasa ile ya basi baada ya kuwa wamewasili Ghana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV