July 25, 2016


Ubovu wa uwanja umesababisha mechi ya watani Manchester United dhidi ya Manchester City kuahirishwa.

Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Bird Nest jijini Beijing, China na ingekuwa ya kwanza kuzikutanisha timu hizo nje ya England.Lakini mvua zilizonyesha mfululizo kwa siku kadhaa, zimechangia kuuharibu uwanja huo.

Mechi hiyo ilikuwa gumzo zaidi kwa kuwa ingewakutanisha Jose Mourinho akiwa na Manchester United na Pep Guardiola akiwa na Manchester City.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV