July 30, 2016


Imani ya mapenzi mashabiki wa Simba imeanza kurejea hasa kutokana na kikosi chao kipya kuonyesha soka safi.

Katika mechi mbili za kirafiki ambazo Simba imecheza mjini Morogoro, imeweza kuonyesha soka safi na kufanya mashabiki kufurahi.


Kuanzia mechi ya kwanza dhidi ya Polisi Moro ambayo walishinda kwa mabao 6-0, halafu wakaitwanga Moro Kids kwa mabao 2-0, ilionyesha wazi kwamba mashabiki hao wamefurahishwa sana.

Ingawa Simba haijaanza msimu lakini soka lake linarejesha imani na mashabiki wa Morogoro wamekuwa wakijitokeza kwa wingi mazoezini licha ya kuwa wanazuiwa kuingia ndani ya uzio, wamekuwa wakibaki nje na kushuhudia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV