July 1, 2016


Katika kuonyesha imedhamiria kufanya kweli kwa ajili ya msimu ujao, Kagera Sugar imefanikiwa kuwanasa wachezaji watano kutoka Mwadui FC, Toto African, Mbeya City na Majimaji.

Imeelezwa kuwa, mazungumzo baina ya wachezaji hao na uongozi wa timu hiyo yalianza mapema mara baada ya kumalizika kwa ligi hiyo na jana Alhamisi kila kitu kilikwenda sawa ikitarajiwa kusainiwa kwa kandarasi leo Ijumaa.

Mtu wa ndani kutoka sekretarieti ya Kagera alilijuza Championi Ijumaa kuhusiana na ishu hiyo na kwamba wamepanga kuwapa kandarasi ya mwaka mmoja kila mmoja kwa ajili ya msimu ujao.

Wachezaji hao ni Themi Felix aliyemalizana na Mwadui hivi karibuni, Edward Christopher na Hassan Khatibu wote kutoka Toto Africans. Wengine ni kipa David Burhani wa Majimaji, Anthony Matogolo wa Mwadui FC waliowahi kuitumikia Mbeya City hapo awali.

Alipotafutwa Mratibu wa Kagera, Mohammed Hussein kuzungumzia suala hilo lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa, alipotafutwa kocha wa timu hiyo, Adolph Rishard naye alieleza kuwa hayupo tayari kuzungumzia masuala hayo.

Alipotafutwa Khatibu, kutolea ufafanuzi ishu hiyo kwa upande wake alisema: “Najua tupo mimi na Edo (Christopher) ndiyo tutakaomalizana na Kagera kesho (leo), hao wengine sijajua na zaidi unaweza kupata ufafanuzi kwa viongozi wenyewe.”


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV