July 21, 2016


Kama ulivyozoea kuwaona akina Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na wengine wakila bata kabla ya kuanza kwa msimu, basi safari hii ni Tanzania, maana mshambuliaji wa Mwadui FC, Paul Nonga ameamua kuichukua familia yake na kwenda kupumzika kidogo mbugani.

Nonga amekwenda kwenye mbuga za Meserani Snake Park iliyoko mkoani Arusha.
Nonga ambaye aliamua kukimbia Yanga na kurejea Mwadui FC, anaonekana ni mwenye furaha akiwa na mkewe na mwanaye wamepanda mnyama ngamia, kwa raha zao.


Kulikuwa na gumzo kubwa baada ya Nonga kuomba kurejea Mwadui FC akiondoka Yanga na ikaonekana aliushindwa mziki wa washambuliaji wawili, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV