July 22, 2016


Baada ya kumaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara kwa kufunga bao moja tu, nahodha na mshambuliaji mkongwe wa Simba, Mussa Mgosi, ametamba kuwa msimu ujao anataka awe mfungaji bora.

Kauli hiyo, aliitoa akiwa kambini mkoani Morogoro ambapo Simba ipo huko ikijiandaa na msimu mpya chini ya Kocha Mkuu Mcameroon, Joseph Omog na Mganda, Jackson Mayanja.

Kauli hiyo ya Mgosi inamaanisha kuwa mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ambaye ndiye alikuwa mfungaji bora hatakuwa na chake msimu ujao.

“Nikuhakikishie tu, mimi ndiye mfungaji bora msimu ujao wa ligi kuu, kwani nina kila sababu ya kutamba hivyo,” alisema Mgosi akionekana kujiamini, kisha akaendelea:

"Unajua msimu uliopita nilikuwa nina majukumu mengi kwenye timu, nilikuwa mshauri wa Kocha Mayanja nikiwa kwenye benchi, hali hiyo ilisababisha kocha asinitumie kila wakati kutokana na majukumu hayo.


“Lakini msimu ujao wa ligi kuu, mashabiki wa Simba watarajie mengi kutoka kwangu, ikiwemo kuifungia mabao ili tufanikishe malengo yetu ya kutwaa ubingwa."

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV