July 22, 2016


Katika kile kinachoonekana tayari uongozi wa Azam FC, umekubali kumuachia mshambuliaji wao, Kipre Tchetche ambaye amekuwa katika mvutano na klabu hiyo, kauli imetoka kuwa straika huyo yupo katika hatua za mwisho kuondoka klabuni hapo rasmi.

Tchetche amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Azam FC lakini hajajiunga kambini huku kukiwa na taarifa kuwa anawaniwa na klabu kadhaa ikiwemo Yanga.

Kaimu Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor amezungumza na gazeti hili na kutoa kauli kuwa kweli wapo katika mazungumzo na moja ya klabu nchini Oman kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo lakini kwa sasa hawezi kuitaja jina kwa kuwa bado mchakato unaendelea.

“Kipre yupo huko (Oman) kwa sasa na tunachosubiri hivi sasa ni fedha ziingizwe katika akaunti ya klabu ili tumruhusu aondoke, kama wakishindwa kutuingizia fedha hizo za usajili, basi hatutatoa ruhusa na tutaendelea kumtambua kuwa ni mchezaji wetu.

“Tumewaambia tunahitaji dola laki moja na nusu (Sh milioni 322) kwa kuwa tunajua kuwa kwa kiwango hicho, hakuna klabu inayoweza kutaka kumsajili hapa Bongo,” alisema.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Henarndez raia wa Hispania amejinadi kuwa hana hofu kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na kudai kuwa timu yake ipo katika mwendelezo mzuri wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.

Akizungumzia mchezo huo utakaochezwa Agosti 17, Zeben alisema: “Natambua juu ya mchezo dhidi ya Yanga lakini siwezi kubabaika kwa sababu ninatengeneza timu yangu, nimeshaona Yanga wakicheza, napambana kuhakikisha wachezaji wangu wanashika vizuri kile ninachowaelekeza, Yanga ni wa kawaida tu."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic