Kujiamini kupindukia kumewaponza Kauzu FC baada ya kuchapwa kwa mabao 3-1 katika mechi ya fainali na Temeke Market ambao wanakuwa mabingwa wapya wa michuano ya Ndondo Cup.
Katika mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye dimba la Chuo cha Bandari maarufu kama Wembley jijini Dar es Salaam, Kauzu waliingia uwanjani na kuanza kucheza kama wana uhakika wa asilimia 100 kupata ushindi.
Lakini baadaye makosa ya safu yake ya ulinzi ulianza kuwagharimu baada ya Madebe kufunga bao la kwanza, Shabani Kisiga ‘Marlon’ akafunga la pili kabla ya Adam Kingwade kumalizia la tatu.
Kauzu walifanikiwa kupata bao la la kufutia machozi katika kipindi cha kwanza katika dakika za nyongeza kupitia Rashid Gumbo.
0 COMMENTS:
Post a Comment