Real Madrid imepewa ofa ya euro milioni 85 kumuuza mshambuliaji James Rodriguez.
Bado haijaelezwa ni timu gani na James raia wa Colombia amethibitisha ofa hiyo lakini amesema kamwe hataki kuondoka Madrid.
“Najua klabu imepata ofa kubwa kuhusiana na mimi, lakini sitaki kuondoka.
“Nataka kubaki haps na kupigania nafasi. Ninaamini nitapambana na kufanikiwa,” alisema akionyesha kujiamini.
James alijiunga na Real Madrid akitokea Monaco ya Ufaransa ingawa bado hajapata mafanikio makubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment