July 25, 2016


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude, amerejea nchini akitokea Afrika Kusini alikodaiwa kwenda kufanya majaribio katika timu ya Mpumalanga Black Aces inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Ingawa hakuwa tayari kuweka wazi kwa sasa kuhusiana na matokeo ya majaribio hayo yaliyochukua takriban wiki tatu, alisema kila kitu kilikuwa sawa na kwamba sasa anajiandaa kujiunga  na kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mkude kufanya kazi na bosi mpya wa benchi la ufundi la timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog kwani awali wakati kocha huyo anaanza kazi kikosini hapo, ndiyo wakati ambao Mkude alitokomea Afrika Kusini.

“Nimerudi juzi na kila kitu kilikuwa sawa na sasa nimerejea, nipo Dar lakini kesho (leo) nitaondoka kuelekea Morogoro kujiunga na timu kwa ajili ya mazoezi. Kwa sasa siwezi kuzungumzia masuala ya matokeo, hayo nitaongelea baadaye,” alisema Mkude.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV