July 28, 2016Kesho ndiyo siku Wanasimba watapata majibu kuhusiana na suala la bilionea Mohammed Dewji na klabu hiyo.

Dewji maarufu kama Mo, aliwahi kutangaza kutaka kuinunua Simba kwa kitita cha Sh bilioni 20 ili apate hisa za asilimia 51.

Lakini kumekuwa bado kuna hali ya sintofahamu na Dewji hajawahi kulizungumzia suala hilo.

Lakini habari za uhakika zinaeleza, kwa mara ya kwanza Mo atafunguka hiyo kesho katika mkutano wa waandishi wa habari.


Taarifa zinasema Mo atazungumza mbele ya waandishi wa habari na kufafanua kuhusiana na jambo hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV