July 28, 2016


Simba imeahidi itawatangaza wachezaji wake wapya na kuwashangaza mashabiki wake siku ya Tamasha la Simba Day.

Tamasha la Simba Day limepangwa kufanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba rasmi itawatangaza wachezaji wake wapya wa kitaifa na kimataifa.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watawashangaza mashabiki wao kwa ‘suprise’.

“Itakuwa ni suprise, kuna wachezaji ambao watatangazwa na kuwashangaza mashabiki wetu. Lakini kila kitu kinakwenda kwa mpangilio safi kabisa.

“Mashabiki wa Simba waje tuungane kusherekea na kuona kikosi chetu,” alisema Aveva.

Tayari Simba imeishatangaza kucheza mechi ya Inter Clube ya Angola ambayo inanolewa na kocha wake wa zamani, Zdravko Logarusic.

Pamoja na hivyo, Aveva alieleza itakavyokuwa wiki ya Simba ambayo itahusisha mambo muhimu kama vile utaoaji damu.

Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.


Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV