Kiungo kinda wa Yanga, Geofrey Mwashiuya amepata msala mwingine baada ya vipimo vya MRI kuonyesha ana ana tatizo la goti linalomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja na nusu.
Mwashiuya tayari ameanza kufanyiwa matibabu jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa daktari wa Yanga.
Kukaa kwake nje, kutamlazimu kuzikosa mechi tano hadi kumi za mwanzo za Ligi Kuu Bara ambayo itaanza rasmi Agosti 20.
Taarifa zinaelezwa, Mwashiuya amewekewa bandeji laini ambayo inamsaidia kupona haraka na imeelezwa aina hiyo ya bandeji ni kama ile aliyofungwa mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy.
.
0 COMMENTS:
Post a Comment