July 3, 2016

OMOG ALIPOWASILI...

Kesho ndiyo Kocha Joseph Omog anaanza rasmi kazi yake ya kuinoa timu yake mpya ya Simba.

Omog ametaka wachezaji wote waliosajiliwa Simba au wanaotarajia kusajiliwa wawe mazoezini bila kukosa.

Omog raia wa Cameroon, ameuambia uongozi angetaka kumuona kila mchezaji wa Simba akiwa mazoezini.

"Kocha anachotaka ni kila mchezaji wa Simba kuwa mazoezini kesho Jumatatu. Anataka kuwaona wachezaji wote bila ya kukosa na kama akianza, aanze moja kwa moja," kilieleza chanzo.

Omog aliwahi kuinoa Azam FC na kuipa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 2014, timu hiyo ilichukua ubingwa bila kupoteza mechi hata moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV