July 29, 2016


Kikosi cha Simba chini ya Joseph Omog kimeendelea kujipima nguvu baada ya kuitwanga Moro Kids kwa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa mjini Morogoro.

Mabao ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib na Danny Lyanga na kuifanya Simba kuandika rekodi ya kushinda mechi mbili za kirafiki mfululizo.

Hii ni mechi ya pili baada ya ile ya kwanza dhidi ya Polisi Moro ambayo Simba ilishinda kwa mabao 6-0.

Katika mechi ya leo, Simba ingeweza kufunga mabao zaidi lakini ilipoteza nafasi kadhaa za kufunga.


Hata hivyo, Moro Kids nao walionyesha soka safi na kuwalazimisha mabeki wa Simba kulazimika kufanya kazi ya ziada, mara kadhaa.

2 COMMENTS:

  1. Katika blog yako neno"rekodi"limepoteza maana yake halisi,yaani timu kushinda mara mbili kwako wewe hiyo ni rekodi!! Ahh brother acha masihara basi.

    ReplyDelete
  2. tatizo mchizi ni mshabiki wa kugalagala wa uongozi wa mbovu kupata kutokea simba,namaanisha uongozi wa AVEVA

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV