July 28, 2016

Ofisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom, Ashutosh Tiwary akimkabidhi Mohamed Hussein Zimbwe mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya mwanasoka bora anayechipukia.


Wakati  msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom  Tanzania bara kwa mwaka 2016/17 ukitarajiwa kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu,  baadhi ya washabiki na vilabu   vinavyoshiriki ligi hiyo vinamuomba mdhamini  mkuu kuangalia namna ya kuvisaidia ili viweze kufaidika zaidi na udhamini wanaoupata.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya washabiki wa mchezo wamesema kuwa kutokana na klabu nyingi kutokuwa na vyanzo vya mapato fedha ambazo vimekuwa zikipata zimekuwa zikiishia kwenya gharama za  kuandaa timu na usafiri  na wachezaji kunufaika kwa kiasi kidogo hivyo kumuomba mdhamini kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

John Msafiri mmoja wa wapenzi wa soka mkoani Mwanza akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa soka ya Tanzania linakabiliwa na changamoto nyingi mojawapo kubwa ikiwa ni klabu za soka kutokuwa na vyanzo vya mapato na kutegemea fedha za wafadhili pekee.

Aliomba zifanyike jitihaza za kukabiliana na changamoto hii  kwa manufaa ya wachezaji na aliwashauri viongozi wa klabu za soka kutobweteka bali kubuni vyanzo vya mapato badala ya kutegemea misaada ya wafadhili kwa asilimia mia moja, kwa kuwa kufanya hivyo kunapunguza mapato ya wachezaji.


Cuthbert  Japhet , Msemaji wa   timu  ya Toto Afrika ya mjini Mwanza amesema kuwa umasikini na kukosa miradi ya maendeleo kwa  klabu ndogo ni moja ya changamoto kubwa inayozikabili  timu maskini na kushindwa kupiga hatua kwa kutegemea fedha ya mdhamini ambayo  haikidhi mahitaji ya timu.

Akizungumza kuhusiana na suala hilo, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa,Victoria Chale alisema kuwa Vodacom kama mdhamini wa ligi imeyapokea maoni hayo kwa ajili ya kuyafanyia kazi  kwa mkataba ujao ili kuboresha ligi hiyo  iwe na mwelekeo  wa kuwanufaisha wachezaji zaidi.

“Mchezo wa soka mbali na changamoto kwaa klabu kutokuwa na vyanzo vya mapato unazo changamoto nyingi ambazo haziwezi kutatuliwa kwa siku moja na zinahitaji jitihada za pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali  wa soka.

Alisema kuwa ufadhili wa Vodacom wa ligi kuu  katika kipindi cha miaka 10 umeleta mafanikio makubwa kwa kuwezesha kuibua vipaji vya wachezaji na kuvikuza na kampuni itaendelea kuboresha udhamini kama ambavyo imekuwa ikifanya mwaka hadi mwaka ili wachezaji pia wanufaike na ushiriki wao katika ligi hii kubwa ya soka nchini.

Aliwataka wadau wengine wajitokeze kudhamini ligi hii ili wachezaji waweze kunuifa na kuboresha maisha yao;

“Mchezo wa soka ni biashara kubwa nina imani makampuni na wadau wengine tukiungana pamoja kwa kutoa udhamini katika vilabu mbalimbali soka yetu itazidi kukua kwa kasi na maisha ya wachezaji kuwa bora zaidi kama walivyo wenzao katika nchi ambazo mchezo huu umekua,” alisema.


Kipenga cha kwanza cha kuashiriria kuanza kwa msimu  mpya wa 2016/2017 kitaanza kupuliza Agosti 17 katika mchezo wa Ngao ya Hisani kwa mabingwa wa Tanzania  timu ya Yanga itakapoivaa timu ya Azam FC yenye makao makuu yake Chamanzi kwenye Uwanja wa Taifa jijiniDar es Salaama

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic