July 30, 2016


Mfanyabishara kijana na maarufu ndani na nje ya nchi, Mohammed Dewji ‘MO’ ambaye ametajwa kutaka kuwekeza kwenye Klabu ya Simba kwa kutoa Sh bilioni 20, jana aliibuka kwenye mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya Moro Kids.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia Highlands, Morogoro uliishuhudia Simba ikishinda mabao 2-0 dhidi ya wenyeji hao na kuwa ushindi wa pili mfululizo baada ya wiki iliyopita kuifunga Polisi Moro mabao 6-0.

Mabao ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 20 akipokea pasi ya Shiza Kichuya na la pili lilifungwa na Danny Lyanga dakika ya 69 akiunganisha pasi ya Mohammed Ibrahim.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliojitokeza uwanjani hapa muda wote wa mchezo walikuwa wakiimba nyimbo za kuushinikiza uongozi umpe timu MO.
Mashabiki hao walisikika wakiimba: “Mo tumpe timu.”


Baada ya mchezo huo Kocha Joseph Omog wa Simba alisema, amefurahishwa na uwezo ulioonyesha na wachezaji wake huku akidai wapinzania wao walikuwa katika kiwango bora tofauti na Polisi Moro ambao waliwafunga 6-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV