July 28, 2016

RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR, LEO. KULIA NI KATIBU MKUU WA KLABU HIYO, PATRICK KAHEMELE.
Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.

Siku kamili ya sherehe itakuwa ni Agosti 8 wakati tamasha la Simba Day litakapofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijiji Dar es Salaam.

“Hii ni kuungana na jamii, tutafanya hivyo katika hospitali mbalimbali ambazo zitatangazwa hapo baadaye,” alisema Aveva.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV