August 1, 2016


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu, amewatangazia vita wapinzani wao Yanga kwa kusema kuwa msimu ujao ni lazima Simba itwae ubingwa wa ligi na kudai kuwa amejipanga kuhakikisha anaonyesha kiwango cha hali ya juu ili kuisaidia timu yake hiyo kufanya vyema.

Simba ilimaliza nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi msimu uliopita huku ikiwa imekosa kucheza michuano ya kimataifa kwa misimu minne mfululizo, hivyo kuifanya timu hiyo iwe katika wakati mgumu.

 Ajibu amesema kuwa, kwa jinsi usajili ulivyofanywa katika kikosi chao, ni wazi ubingwa utakuwa wa kwao msimu ujao kutokana na kila mmoja kujituma lakini alidai tuzo aliyoipata ya mfungaji wa bao bora la msimu, itampa chachu ya  kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

“Wanasimba watarajie mambo mazuri msimu ujao wa ligi kuu ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa kwani ndiyo dhamira yetu kutokana na usajili mzuri ambao umefanyika.

“Najipanga kuhakikisha naendelea kuwa katika kikosi cha kwanza kwani ushindani umeongezeka kwa sasa. 

Atakayejituma ndiye atakayepata nafasi kwa kuwa kocha mpya Joseph Omog hamjui mchezaji yeyote, hivyo ni nafasi kwa wachezaji kuhakikisha kila mmoja anaonyesha uwezo wake ipasavyo ili kuweza kumshawishi kocha kumpa nafasi na kuondokana na malalamiko ya kutopangwa katika kikosi cha kwanza,” alisema Ajibu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV