August 1, 2016


Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amepata pigo kufuatia kufiwa na baba yake mzazi, mzee Fakehe Juma aliyekuwa akiishi mkoani Tanga.

Pondamali alikuwa nje ya nchi wakati msiba huo unatokea wakati timu yake ya Yanga ilipokuwa ikicheza na Medeama ya Ghana katika mchezo wa marudiano na kujikuta ikichapwa mabao 3-1.

Pondamali ameeleza kuwa, alipigiwa simu alipokuwa Ghana kufahamishwa juu ya msiba wa mzazi wake huyo, hivyo ilimlazimu kwenda kuhani mara tu baada ya kuwasili Bongo.

“Kwa sasa mimi sipo na timu kwa kuwa nipo Tanga kuja kuhani msiba wa baba yangu mzazi mzee Juma wakati nipo Ghana, hivyo nilivyofika airport nilipitiliza moja kwa moja hadi huku.

“Ni pigo nililolipata ila namshukuru Mungu kwani ndiye muweza wa yote, natarajia kuwasili Dar wiki ijayo ili kuendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya MO Bejaia na kwa upande wa makipa wangu wako fiti,” alisema Pondamali.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic