August 26, 2016


Kikosi cha Azam FC kimeendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ya Songea.

Mechi hiyo itakuwa ni ya kujirekebisha kwa Azam FC baada ya kuanza ligi kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon iliyorejea ligi kuu.

Nafasi nzuri ya Azam FC kujirekebisha ni Jumamosi dhidi ya Majimaji mechi itakayopigwa kwenye uwanja huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV