August 26, 2016Wabunge wa vyama mbalimbali ambao ni mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba, leo wametoa msimamo wao kuhusiana na ombi la mfanyabiashara Mohammed Dewji kutaka kuinunua klabu ya Simba kwa asilimia 51.

Wabunge hao wakiwemo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walitoa msimamo wao walipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, leo.

Mo Dewji ametenga kitita cha Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo.

Wabunge hao wakiongozwa na Juma Ngamia, Adam Malima na Profesa Jay wamesema wanaamini hilo ni jambo zuri.

Wamesisitiza Simba inachotakiwa ni kuangalia huu ni wakati mwafaka wa maendeleo na mabadiliko ambayo yatakuwa na tija.

Wamewataka Wanasimba kutoa ushirikiano katika suala hilo la Mo Dewji ili kuisaidia klabu hiyo kubadilika baada ya kuwa imesota miaka minne sasa bila ya ubingwa wala kucheza michuano ya kimataita.

Mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa wakiunga kwa nguvu kuhusiana na Mo Dewji kununua hisa hizo ili kuchangia mabadiliko ndani ya klabu hiyo.

Katika mkutano wa wanachama hivi karibuni, wanachama waliucharukia uongozi wakitaka upitishe mabadiliko hayo ili Simba itoke kwenye wimbi la kuwa msindikizaji na kurejesha heshima yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV