August 26, 2016


Beki wa kati wa Azam FC, Serge Wawa sasa anaonekana yuko fiti asilimia 100 na wakati wowote ataanza kukitumikia kikosi chake.

Wawa ameonekana akipasha mazoezini na wenzake huku akionekana yuko fiti na tayari kwa mechi ya kesho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ya Songea.

Beki huyo alisafirishwa kwenda kupata matibabu nchini Afrika Kusini. Baadaye akasafiri hadi kwao Ivory Coast kwa ajili ya mapumziko.

Kurejea kwake kutakuwa ahueni kwa safu ya ulinzi ya Azam FC ambayo inaonekana kusakamwa na majeruhi wengi.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV