August 11, 2016



HASSAN DALALI (MWENYE KIBARAGASHIA) AKIWA NA BAADHI YA WANACHAMA WA SIMBA.
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema amefurahishwa na watani wao Yanga kutaka kukodishwa na mwenyekiti wao, Yusuf Manji.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Dalali amesema anatanga kuanza kuwakodisha Yanga viti vyao ili kuvitumia katika sherehe mbalimbali.

Amesema anavyotaka kukodisha yeye, ni vile ambavyo aliyetangaza kukodisha yaani Manji, ameviacha.

“Nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa watani zetu wenyewe wanakwenda na mambo ya kukodisha, ninajua wana viti vingi pale, sasa nataka kukodisha.

“Wameamua kufanya biashara ya aina yake, nafikiri itakuwa ya kwanza. Sasa mimi nikikodisha viti kwao kwa miezi kadhaa, nafikiri itakuwa haina tofauti na wanavyokodisha timu. Wao ni wajasiriamali,” alisema Dalali na kucheka.


Manji ametangaza kutaka kuokodisha timu ya Yanga na nembo ya klabu kwa miaka 10 na faida asilimia 75 kama itapatikana atachukua na 25 utachukua uangozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic