Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema tayari ameandika barua kwa uongozi wa Simba kueleza kuhusiana na uamuzi wake wa kutaka kununua hisa za Simba kwa asilimia 51.
Mo amesema ameandika barua hiyo leo asubuhi baada ya kusikia baadhi ya viongozi wa Simba wakisema hakuwa amefanya hivyo.
"Kweli hatukuwa tumeandika barua kwa kuwa nilitaka mchakato uchukue hatua. Baada ya hapo lingefuata suala labarua, lakini kwa kuwa wanasema lazima barua, basi acha tufanye hivyo.
"Tayari barua imeandikwa na imepelekwa kwenye klabu, kukawa hakuna mtu na sasa imepelekwa ofisini kwa Aveva," alisema Mo.
"Nilichoeleza kwenye barua yangu ni kilekile kwamba ninatoa ofa ya Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51. Niko tayari kushirikiana na uongozi wakati wa mchakati kama ambavyo nilieleza awali," alisema.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMABADILIKO KWA WANASIMBA NI LAZIMA
ReplyDeleteMimi natoa jibu leo nani anyesema hafaham maana ya Hisa?, Hisa maana yake ni Biashara ya kumiliki kitu au kampuni kwa kununua na kumiliki na Endapo kuna mtu atakua na pesa anataka kununua kiasi cha Hisa kwa mtu huwa akaliwi, kwahiyo kama MO atapewa timu pia mtu mwingine akajitokeza kununu Hisa anaruhusiwa kununua, na Mimi naomba niwaulize wale mnapinga hili je, nilini wanachama wamekuua juu ya viongozi zaidi ya kuwa na haki ya Kushangilia au Kuzomea tu, ninani yupo Tayari kuchangia 3000 tu kila mwezi kwaajili ya Timu wakati mtu anajiita mwanachama kadi halipii mpaka siku ya Mkutano, Tuache kuwabeba wanaotuumiza kilasiku siasa haziitajiki katika soka, Au mnapenda tuwe tunawanyenyekea wazamini na wazili kwa pesa zao, Ndio maana leo TBL tunamnyenyekekea anatuambia hawezi kutuzamini mpaka na Yanga wakubali udhamini huo kisa kuogopa ushindani wa kibiashara endapo Yanga akichukuliwa na wapinzani wake kwenye biashara mbona Barcelona na Real Madrid wazaminiwi na kampuni moja japo ni wapinzani City na United hivyo hivyo pia, Tuipeleke tim mfumo wakibiashara pia tutazuia hata uingizaji wa jezi feki zinazouzwa mitaani kwasababu hiyo pia ni kazi ya kamputi ili iingize mapato nani anauhakika lile duka linalouza vifaa vya Simba ni mali ya club?, Hivi mnarizika ligi nzima jezi zinafanana kasoro rangi tu, leo jezi ya Simba na Coastal zinatofautiana nembo tu,Tukubali mabadiliko ili tuwe hata na Uwanja ambao utaingiza pesa kupitia matangazo yatakayowekwa pembeni ya uwanja si lazima awe mdhamini. Simba, Nguvu moja