August 17, 2016


Kama umebahatika kuyashuhudia mazoezi ya kikosi cha Simba, ni lazima umuonee huruma kiraka wa siku zote, Awadh Juma ‘Maniche’. Amekuwa akipigwa benchi hadi kwenye mechi za mazoezini wakati mwingine kutocheza kabisa.

Hata hivyo, kocha mkuu, Joseph Omog ameamua kutolea ufafanuzi sababu za kutomtumia kiungo huyo maarufu kama ‘nyota wa Mtani Jembe’ aliyeifunga Yanga mechi zote na kuinyima mamilioni ya fedha katika mechi za mbili za Mtani Jembe.


Omog amesema : “Hapana siyo kwamba hayupo kwenye mipango, nimemkuta akiwa mgonjwa, nilielezwa aliumia mwishoni mwa msimu uliyopita na bado hajawa fiti ndiyo maana nampumzisha kwa sana hata mazoezini.”

Kwa kauli hiyo yan Omog, maana yake Juma ana nafasi bado, kwani atakapopona vizuri ana nafasi ya kuonyesha uwezo alionao na kocha huyo ataamua cha kufanya.

Juma amekuwa ni kiraka na mchezaji muhimu katika kikosi cha Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV