August 17, 2016Hii kali, yule kiungo wa Coastal Union, Mcameroon, Youssouf Sabo, aliyeifunga Simba mabao mawili katika mchezo wa Kombe la FA hatua ya robo fainali msimu uliopita? Sasa licha ya kuwa na uwezo mkubwa, amekosa timu ya kuichezea katika Ligi kuu Bara msimu ujao 

inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20, mwaka huu.
Kiungo huyo ambaye alitokea katika timu ya Coton Sports ya nchini kwao, licha ya kuwa na uwezo mkubwa, lakini hakuweza kuinusuru Coastal Union kushuka daraja msimu uliopita huku akikumbukwa na mashabiki wa Simba kutokana na kuwaondoa kwenye Kombe la FA kufuatia mabao yake mawili.

Amesema licha ya dirisha la usajili kwa wachezaji wa kimataifa kuwa bado halijafungwa, alisema amepanga kutimkia nyumbani kwao kuangalia mipango mingine.

“Kiukweli bado sijapata timu ya kuichezea msimu ujao kwani mipango yangu ya awali ilivurugika, hivyo naamini sitacheza msimu ukianza kitu ambacho siyo kizuri kwangu, ingawa dirisha la usajili kwa wachezaji wa kimataifa bado halijafungwa, lolote linaweza kutokea.

“Naendelea kufuatilia fedha zangu ninazowadai Coastal huku nikiwa nafanya mipango ya kurejea kwetu Cameroon kutafuta timu ya kuichezea,” alisema Sabo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV