Beki wa kulia wa Azam FC, Shomari Kapombe sasa yuko safi na anaweza kuanza kuitumikia Azam FC wakati inaivaa URA, kesho.
Azam FC inaivaa URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema, Kapombe sasa yuko fiti baada ya matibabu na baadaye kuungana na wenzake kikosini.
"Kapombe yuko safi sana, tena sasa hivi anaonekana ni zaidi. Nina imani mwalimu atampanga katika mechi dhidi ya URA," alisema.
Kapombe aliunga na kikosi hicho na makocha kutoka Hispania walikuwa wakimpa mazoezi maalum kuhakikisha anakuwa fiti kwa kuwa aliongezeka sana uzito.
0 COMMENTS:
Post a Comment