Beki wa kati wa Azam FC, Paschal Wawa amerejea kikosi na kuanza mazoezi na wenzake.
Wawa raia wa Ivory Coast alikuwa majeruhi na amekaa nje ya kikosi hicho kwa zaidi ya miezi miwili.
Lakini kuanzia leo, ameungana na wenzake na kuanza mazoezi ya taratibu akiwa njiani kurejea kikosini.
Baada ya kutoka Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu, Wawa alisafiri kwenda kwao Ivory Coast kwa ajili ya mapumziko.
0 COMMENTS:
Post a Comment