August 26, 2016

GONZALEZ AKIWA WEST HAM

Kipa Juan Jesus Gonzalez raia wa Hispania ambaye alionekana hafai katika kikosi cha Azam FC, ameanza majaribio katika kikosi cha West Ham United ya England.

Gonzalez ambaye alifanya majaribio Azam FC, lakini kukawa na taarifa kuwa uongozi ulionekana kutofurahishwa naye, ameanza majaribio katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Taarifa za ndani zinaeleza, kipa huyo ameanza rasmi mazoezi jana na ameonyesha uwezo mzuri.

GONZALEZ AKIWA NA MSEMAJI WA AZAM FC, JAFFAR IDDI MARA TU BAADA YA KUTUA NCHINI KWA AJILI YA MAJARIBIO.
“Bado West Ham hauitazungumza suala la kipa huyo kwa kuwa ndiyo ameanza majaribio,” alisema Jonas McJones ambaye ni mmoja wa wanaohusika na kitengo cha habari.

Gonzalez alitua nchini akitokea Tenerife ya Hispania na kufanya majaribio. Lakini mwisho, aliondolewa baada ya kuwa na taarifa kwamba viongozi hawakufurahishwa naye licha ya Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania kuonekana kufurahishwa naye.


3 COMMENTS:

  1. Soka la bongo ni shida ina maana uongozi na kocha nani anajua mchezaji gan anafaaa na yupi hafai?.salehjembe

    ReplyDelete
  2. Hapana tusihukumu na kutoa lawama kwa timu. Inatupasa kufahamu taarifa tunapata kwa nani hasa, je mtoa taarifa ni sahihi kwenye timu tunayozungumzia?

    ReplyDelete
  3. Nafikiri waliona siyo vema kwa timu kujaza wachezaji wengi kwenye namba moja, badala yake waweze kuongeza wachezaji kwenye namba nyingine.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV