August 14, 2016



TP Mazembe imekubali kipigo cha mabao 3-2 ikiwa ugenini dhidi ya Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho, leo.

Ushindi huo wa Medeama, maana yake imefikisha pointi 8 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga huku Mazembe ikiwa kileleni na pointi 10.

Baada ya ushindi wa Medeama, maana yake rasmi Yanga ambayo jana iliifunga Mo Bejaia imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kuwa na mchezo mkononi.

Yanga inabaki na pointi nne mkiani, huku Mo Bejaia ikilazimika kutupa karata yake ya mwisho kwa kutaka kuifunga Medeama katika mechi ya mwisho ili ifikishe pointi nane huku ikijaribu kuangalia wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya TP Mazembe ikiwa ugenini mjini Lubumbashi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV