August 17, 2016

Kiungo mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez ameweka wazi kuwa yupo tayari kuondoka klabuni hapo ikiwa atapata ofa kutoka Real Madrid au Barcelona.

Mchezaji huyo ambaye anahusishwa kusajiliwa na Arsenal, alinukuliwa akisema hivi karibuni kuwa ataendelea kubaki klabuni kwake lakini kama ikija ofa kutoka moja ya timu hizo mbili kubwa za Hispania ataifikiria.

  “Natamani kuendelea kucheza hapa (Premier League) kwa muda mrefu lakini kwa sasa kuna klabu mbili au tatu ambazo zikija siwezi kusita kuzifikiria, nafikiri naeleweka ninachokisema.”

Mbali na hapo, Mahrez amefikichua kuwa staa wa Barcelona, Lionel Messi alimpongeza kutokana na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa England msimu uliopita. Anasema pongezi hizo alimpa wakati walipokutana katika mechi ya kirafiki hivi karibuni.

Msimu uliopita Mahrez alifunga mabao 17 katika Premier League na kutoa asisti 11 lakini kwa sasa bado kasi yake haijachanganya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV