August 17, 2016Na Saleh Ally, Barcelona
Barcelona itamkosa mkongwe Andres Iniesta wakati inaivaa Sevilla katika mechi ya pili ya Super Cup ya Hispania, hapa maarufu kama Supercopa de Espana kwenye wa Camp Nou jijini hapa, leo.

Maana yake, heshima ya kitambaa cha unahodha inakenda kwa Lionel Messi ambaye kama watashinda kombe hilo, itakuwa ni mara yake ya kwanza kubeba kombe akiwa nanodha.

Iniesta ni majeruhi na atakuwa jukwaani akiwashuhudia wenzake wakipambana. Messi atakuwa uwanja akiwaongoza wenzake ili waanze msimu na kombe mkononi.

Katika mitaa mbalimbali ya jiji la Barcelona, gumzo ni mchezo huo na mashabiki wake wanaonekana kutokuwa na hofu hats kidogo na Sevilla.

Lakini baadhi wanaamini Sevilla si timu ya kubeza hats kidogo, hivyo ni lazima wapambane kweli.


Tokea msimu wa 2004-05, Messi ndiyo alianza kucheza fainali ya kombe hilo, lakini leo kwake itakuwa ni heshima zaidi kwa kuwa mkononi ana kitambaa cha unahodha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV