August 29, 2016

BAADHI YA MASHIBIKI WA SIMBA AMBAO HUSHANGILIA KWA AMANI UWANJANI.

Katika hali isiyotarajiwa, makomandoo wa Simba juzi Jumamosi walitaka kuchezea pabaya baada ya kuzinguana na wanajeshi wa JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa suluhu, kisa kikiwa ni vyumba vya kubadilishia nguo.

Mazoea ya timu za Simba na Yanga kujipangia vyumba vya kubadilishia uwanjani hapo, bila kutumia sheria ndiyo yalikuwa chanzo cha yote ambapo makomandoo waliwahi mapema kuandaa mazingira katika vyumba ambavyo kisheria vilitakiwa vitumiwe na maafande hao, lakini baadaye walitaka kubadilisha ndipo mtiti ulipokuja.

Katibu wa JKT Ruvu, Ramadhan Madoweka, amefunguka mkasa mzima katika mahojiano na Championi Jumatatu:
“Ni kweli kulitokea kutofautiana kabla ya mchezo. Watu wengi hawajui sheria, mfano kama hao makomandoo.

 "Timu mwenyeji (katika mchezo huo walikuwa JKT) anatakiwa kukaa kushoto mwa uwanja, tulipokuja tulikuta Makomandoo wameshaingia kwenye vyumba vyetu, hatukutaka shida, tukachukua vya timu ngeni.

“Baadaye wao walikuja wakitaka kubadilisha vyumba, wakitaka wahamie vya timu ngeni ambavyo kisheria vilikuwa vyao lakini walishachukua vyetu, tukawaambia wakae hukohuko maana wao ndiyo walianza kuvunja sheria, wakang’ang’ania na sisi tukawaweka MP (Military Police) kuvilinda. Lakini baadaye walikuja kwa upole na tukaelewana kauli, tukawaruhusu tubadilishane,” alisema Madoweka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV