August 29, 2016Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amesema kuwa anataka kuwa kama mwanariadha machachari duniani Usain Bolt ambaye amekuwa akiandika rekodi mbalimbali katika mashindano anayoshiriki.

Kutokana na hali hiyo, Tambwe naye amedai kuwa anataka kuandika rekodi nyingine msimu huu ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine tena endapo Mungu atamjalia uzima.

Amedai kuwa uamuzi huo umekuja hivi karibuni baada ya kuona uwezo wa washambuliaji wengine waliokuwa wakimtishia amani kuwa ni wa kawaida sana.

Tambwe amesema kuwa hapo awali alikuwa na hofu juu ya hilo lakini kwa sasa amegundua kuwa anaweza kufanya hivyo endapo Mungu atamjalia uzima kutokana na kuwaona wapinzani wake hao uwanjani, akiwemo Mrundi wa Simba, Laudit Mavugo jinsi wanavyocheza.

BOLT
“Kumbe ninaweza kuwa bingwa wa rekodi kama Usain Bolt endapo Mungu atanijalia uzima kwa sababu ile hofu ya kutetea tuzo yangu ya ufungaji bora imeondoka kabisa baada ya kuwaona washambuliaji wengine waliokuwa wakinitishia amani, akiwemo Mavugo.

“Kutokana na hali hiyo napenda kusema kuwa nipo tayari kutetea tuzo yangu hiyo ila jambo kubwa namuomba Mungu anijalie uzima,” alisema Tambwe ambaye ana rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara mara mbili tangu alipotua hapa nchini msimu wa 2013/14 akitokea Vital’O ya Burundi

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV