August 8, 2016


Simba inaongoza kwa bao 1-0 katika mechi ya Simba Day dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Mechi hiyo inachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na bao la Simba limefungwa na Ibrahim Ajib katika dakika ya 38.

Ajib alipokea pasi ya Moussa Ndusha raia wa DR Congo na akiwa umbali wa zaidi ya mita 24 aliachia shuti kali la chinichini lililojaa wavuni.

Simba imeonyesha soka safi tokea mwanzo ingawa inaonekana kutokuwa na maelewano mazuri hasa katika hatua za mwisho au umaliziaji.


Leo Simba inasherekea miaka 80 tokea ianzishwe 1936 na kuna keki maalum ambayo italiwa wakati wa mapumziko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV